![]() |
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ABDULRAHMANI KINANA |
Wakizungumzia hali hiyo mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ABDULRAHMANI KINANA alipofanya ziara ndani ya bonde hilo , wakulima hao wamesema hatua ya ujenzi wa uzio huo umeweza kuwasaidia kunusuru mazao yao yaliyokuwa yakiathiriwa na maji chumvi yaliyokuwa yakiingia ndani ya bonde hilo kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Uzio huo utawawezesha wakulima wa bonde la KOOWE kuzalisha nafaka za mazao mbalimbali ili hali hiyo isiendelee kuathiri rasilimali za ardhini ambazo zimekuwa zikitoweka kutokana na uharibifu wa mazingira hasa ukataji wa mikoko.
Wakizungumzia kitaalamu kuhusu tatizo hilo baadhi ya wataalamu wa Kilimo na Maliasili na Uwagiliaji maji wamesema kuwa tatizo hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayosababisha bonde hilo hapo mwanzo kingiwa na maji ya chumvi kutokana na ukataji ovyo wa mikoko baharini
No comments :
Post a Comment