![]() |
Simba wanaopanda juu ya miti - Wanaongeza umaarufu wa Hifadhi ya Ziwa Manyara |
Haya ndiyo mambo ambayo tuliyojifunza tukiwa ziarani ndani ya Hifadhi ya Ziwa Manyara.
1. Masharti ndani ya Hifadhi
Mtu yeyote anapokuwa ndani ya Hifadhi anatakiwa kufuata masharti au sheria hizi: kuwa kimya kadri iwezekanavyo, kutotupa takataka ndani ya hifadhi, kutochoma moto, kukata miti au kuni, kutowakaribia wanyama pori, kutoshuka ndani ya chombo cha usafiri na kutokuwinda, kuua wanyama au kuchukuwa kitu chochote.
2. Asili ya neno Manyara
![]() |
Mti wa Mnyaa |
![]() |
Mti wa mnyaa |
Neno Manyara limetokana na neno la jamii ya Kimasai (Imanyara). Kwa Kiswahili unaitwa mnyaa. Kwa kawaida mmea huu unatumika sana kwa wigo kuzunguka boma. Mnyaa ni mmea wa asili ambao kwa Kisayansi unaitwa euphorbia tirucalli. Kwa hiyo wageni wengi walishindwa kutamka neno hilo na kutamka MANYARA
3. Miamba, kingo kali na bonde lenye Ziwa
Miaka milioni tatu iliyopiza dunia ilichanika na kupelekea sehemu ya ardhi kudidimia na kufanya bonde la ufa ambalo ni kubwa lenye urefu wa kilometa. Maji ya mvua yanayotiririka kwenye bonde hili hayana pa kutokea hivyo hujikusanya bondeni na kufanya Ziwa. Manyara, Natroni, Nyasa na Rukwa ni baadhi ya maziwa ya aina hii ya bonde la ufa.
4. Makazi ya wanyama pori katika Hifadhi ya Ziwa Manyara.
Makazi ya hifadhi hii ni kama vile: ufukwe wa ziwa, msitu wa maji ardhini, vichaka vya migunga, mbuga wazi, ukuta wa bonde la ufa na ziwa lenyewe
5. Wanyama waliopo ndani ya Hifadhi ya Ziwa Manyara
Baadhi ya wanyama hao ni:-
i. Nyani(Olive baboon). Kundi la nyani huwa na nyani kati ya 30 - 100 wazima, madume, majike, vijana na watoto
ii. Tumbili(vervet monkey): Hawa hupendwa kuwindwa na chui kama chakula chao.
iii. Kima (blue monkey): Huyu ni mzito kuliko tumbili
iv. Nguchilo (Banded Mangoose). Huishi kwenye mapango. Hutoka kwenda kutafuta chakula na kuingia kwenye pango jingine na hupendelea kuishi katika makundi ya 30.
v. Ngiri (warthog): Ngiri ni wachangamfu wakati wa mchana, usiku huchimba mahandaki na kuingia humo kinyume nyume ili kujiweka tayari kujitetea kwa meno yao marefu na makali dhidi ya maadui wao.
vi. Swala/paa (Impala): Huishi kwa kula majani ya miti na majani - nyasi fupi. Huishi katika jamii yenye majike wengi, watoto wengi na dume moja mtawala. Aidha ukikuta dume pekee yao basi huenda wakawa kati ya 10 - 50 idadi yao.
vii. Pundamilia (zebra): Pundamilia hupendelea maeneo ya wazi yenye nyasi fupi. Hula majani - nyasi tu.
viii. Nyati/mbogo (buffalo): Wanyama hawa hufafana sana kama ng`mbe. Nyati hula majani tu. Hupendelea kula usiku na kutafuta maji kando kando mwa ziwa au kwenye matindiga. Pia hupenda kucheza kwenye matope.
ix. Twiga (Maasai giraffe): Twiga chakula chake kikuu ni majani na mbegu za miti ya migunga.
x. Tembo (elephant): Tembo huishi katika familia moja moja na kwa karibu sana. Tembo jike anaanza kuzaa aikwa na umri wa miaka 12. Umri wa kuishi kwa tembo ni miaka 60.
xi. Kiboko (Hippopotamus). Miili yao mikubwa ni kero wakari wa jua kali. Kutokana na hali hiyo mchana kutwa huwa wanajizamisha ndani ya maji. Usiku wanatoka kwenda kutafuta chakula. Kiboko hula majani tu.
xii. Simba (lion): Simba hutumia muda wote wa mchana kwa kulala, kucheza, kugaragara, kupumzika au kusalimiana. Kwa kawaida simba huwinda usiku.
xiii. Ndege. Katika hifadhi hii kuna ndege wengi zaidi ya 400. Baadhi ya ndege hao ni: Kung`wani (crowned crane), heroe mdogo (lasser flamingo), heroe mkubwa (greater flamingo), Mumbi (ground hombill), hondohondo (hombills), deterpwani (pied kingfish), johari (pelicans) nk.
Hapa juu nimeandika baadhi ya wanyama tu wapo zaidi ya hao.
Mbali na wanyama hifadhi hii ya Ziwa Manyara kuwa na wanyama pia ina vivutio vingine kama vile chemchemi ya maji moto, msitu wa maji ardhini - hufanya hifadhi ioneka na ukijani wakati wote, mti wenye sumu kali, ziwa lenyewe, kingo zake nk.
MWISHO
Niwashukuru wadau wote waliofanikisha ziara hiyo.
Damian Mkongwa
Mratibu wa ziara
0784161644/753838499
3. Miamba, kingo kali na bonde lenye Ziwa
Madhari ya Hifadhi ya Ziwa Manyara |
4. Makazi ya wanyama pori katika Hifadhi ya Ziwa Manyara.
![]() |
Ndege wanaolipamba Ziwa Manyara |

No comments :
Post a Comment