SHULE YA WASIOONA IRENTE
YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO KATIKA HIFADHI YA ZIWA MANYARA ILIYOFANYIKA TAREHE 9 –
11/7/2014
Shule ya msingi ya
wasioona Irente yafanya ziara ya mafunzo katika Hifadhi ya Ziwa Manyara. Safari
ilianza tarehe 9/7/2014 shuleni hapo na kuwasili Mto wa Mbu ambapo ndipo makao
makuu ya Hifadhi hiyo yalipo.
Wanafunzi walipewa
maelekezo mahali walipo na pana nini. Nilifurahi zaidi pale walimu walipoanza
kuleza wanafunzi kwamba tunamalizia safu za milima ya Usambara na tunaanza safu
za milima ya Pare. Mwalimu aliwambia wanafunzi kuwa kuna bonde lililotenganisha
safu za milima ya Usambara na Pare. Mwalimu aliendelea kufafanua kuwa ukifuata
bonde hilo utakutana na Hifadhi ya Mkomazi ambayo ipo katika mikoa miwili yaani
Tanga na Kilimanjaro.
Mara baada ya kufika Hai
mkoani Kilimanjaro wakaamua kupata chochote kwa uhai na ustawi wa mwili. Hivyo
wakaingia katika Hoteli inayoitwa WESTLIFE VIP GARDEN
Tazama picha hapa chini.
Mara baada ya kuwasili
katika Hifadhi ya Ziwa Manyara walipokelewa vizuri na kuoneshwa mahali pa
kulala. Wanafunzi waliwaona wanafunzi wengine waliofika Hifadhini hapo kwa
Ziara za Mafunzo ambao nao waliitumia Hosteli hiyo hiyo. Walimu wakatoa elimu
ya mazingira na ujongeaji kwani kwao yalikuwa mazingira mapya na yalihitaji
uangalifu wa hali ya juu wakati wa kutembea.
Picha za hapa chini zinaonesha wanafunzi wakiwa katika Hosteli ya Hifadhi ya Ziwa Manyara
Hapa chini ni viwanja vya michezo vilivopo karibu sana na Hosteli ya Hifadhi ya Ziwa Manyara
Wanafunzi wakifanya mazoezi kwenye bembea
Wananfunzi wakiwa na mwalimu wa Jiografia katika eneo la Chemchem ya Maji ya moto
Wanafunzi wakiwa eneo la Maji moto
Mwalimu wa Jiografia akishikilia fuvu la kichwa la nyani
Mwalimu mtaalamu akifurahia kuwepo kwenye eneo lenye maji ya chemchem ya moto
Nyani akiangalia wageni waliotembelea Hifadhi ya Ziwa Manyara
Wanafunzi wakipata chakula cha mchana ndani ya Hifadhi na kuwasikiliza waongozaji wakati wa kufanya majumuisho kwa makundi yote mawili
Wanafunzi wakifurahia chakula cha mchana ndani ya Hifadhi
Wanafunzi na watalii kutoka nje ya nchi wakiwa katika eneo maarufu sana kwa wanyama aina ya VIBOKO
Wanafunzi na watalii wengine wakigusa maji ya moto yatokayo ardhini
Twiga wakiwa katika maeneo yao ya kujidai
Nyati na ndege wakiwa pamoja
Mkuu wa msafara akifurahia kuwepo muhimu ndani ya hifadhi
Aina mojawapo ya ndege wanaopamba Ziwa Manyara
Wanafunzi wakipapasa na kugusa ngamia Snake Park - Arusha
Geti ya kuingilia Hifadhi ya Ziwa Manyara
Wanafunzi wakigusa na kuchunguza kinyago cha tembo - Mto wa mbu
Mwalimu mkuu akiwagusisha wanafunzi baadhi ya silaha za jadi - Mto wa Mbu
Wanafunzi wakipapasa kinyago cha twiga akinyonyesha mtoto
Wanafunzi wakipapasa kinyago cha tembo - Mto wa Mbu
Wanafunzi wakifurahia kuona na kusikia mlio wa mamba - Snake Park Arusha
Nyani akisalimiana na wanafunzi Snake Park Arusha
Mamba akiwa ndani ya wigo Snake Park Arusha
PONGEZI NA SHUKRANI
Tunapenda kutoa pongezi na shukrani kwa wadau wote waliofanikisha Ziara hii ya mafunzo katika Hifadhi ya Ziwa Manyara.
Mungu awabariki kwa moyo huu.
No comments :
Post a Comment