Wednesday, August 27, 2014

KUAMINI RIPOTI ZA HABARI

Katika ulimwengu huu tunaoishi una maendeleo ya hali ya juu sana ambapo yamkini ni zaidi ya enzi za Musa katika maandiko matakatifu. Hivyo kutokana na maendeleo yaho leo hii yametuweka mahali ambapo dunia tunaiona kama kijiji. Kinachotupelekea kuona dunia ni kama kijiji hasa pale jambo linatukia Marekeni au nchi fulani na jambo hilo hilo tutalisikia na sisi hapa kwetu Tanzania.

Waandishi wengi wa habari na mashirika yaliyowaajiri wanasema wajibu wao ni kutoa ripoti sahihi.Kutotewa ama kutotolewa habari fulani kunategemea sana mambo yafuatayo:-


1. Wamiliki wa vyombo vya habari
2. Serikali
3. Matangazo ya biashara
4. Mapenzi ya mwandishi wa habari
5. Uaminifu wa mwandishi wa habari
6. Mashindano
7. Makosa

Ili tuweze kuamini habari fulani ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:-

1. Chanzo
Habari hiyo inatoka kwa mtu au shirika linaloaminika? Je chapisho hilo au programu hiyo inajulikana kwa kutoa habari zinazoaminika au kusisimua tu? Shirika hilo linadhaminiwa na nani?

2. Utafiti
Maswali mengi hapa tunatakiwa kujiuliza kabla ya kuiamini habari yoyote ile kama vile:- Je habari hiyo imefanyiwa utafiti wa kutosha? Je inategemea chanzo kimoja tu? Je vyanzo vya utafiti vinatoa habari bila ubaguzi na vinachunguza mambo kwa akili pana tu? Je vina maoni yenye usawa au vinatoa maoni ya upande mmoja tu?

3. Kusudi
Jiulize: Je habari hii imekusudiwa kuelimisha au kufurahisha tu? Je mwandishi anajaribu kuuza kitu fulani au kuunga mkono jambo fulani?

4. Hisia
Habari inayoonesha hisia za hasira, dharau au kuchambua inaonesha kwamba imekusudiwa kushambulia na si kutoa hoja zinazopatana na akili.

5. Upatano
Je habari hiyo inapatana na habari zilizo katika ripoti au makala nyingine? Ikiwa habari hiyo inakinzana  basi jihadhari au tahajudi!

6. Imepitwa na wakati
Jambo ambalo lilidhaniwa sahihi miaka 20 iliyopita huenda lisiwe sahihi leo hii. Na hapa simaanishi sana kuwa habari inaweza ikawa ya leo lakini isiwe sahihi au ya kuaminiwa. Hapa kila mtu anatakiwa ajihadhari sana na kuchunguza ukweli wa mambo/habari husika.

Baada ya kufanya mambo ambayo nimeyaorodhesha hapo juu ndipo unaweza kuchukua uamuzi wa kuamini au kutoamini ripoti ya habari fulani. 


No comments :

Post a Comment