Wednesday, June 13, 2018

Mbuga ya wanyama pori ya Serengeti ndio bora zaidi Afrika 2018

www.fahamuhaya.blogspot.com

Mbuga ya wanyama pori ya Serengeti ndio bora zaidi Afrika 2018


Mbuga ya kitaifa ya wanayama pori ya Serengeti nchini Tanzania imeibuka ya kwanza Afrika baada ya utafiti uliofanywa na kampuni ya utalii ya Safari Bookings, utafiti uliofanyika mtandaoni kupitia tovuti yake.
Wanyama wakiwa katika hifadhi ya Serengeti
Image captionWanyama wakiwa katika hifadhi ya Serengeti
Hifadhi hiyo imepata alama 4.9 kati ya 5. Mwaka 2015 Serengeti ilishinda na kuwa hifadhi bora zaidi.
Miongoni mwa mbuga tatu bora ni pamoja na hifadhi ya Mala Mala nchini Afrika Kusini na Hifadhi ya Mana Pools ya nchini Zimbabwe.
Utafiti ulihusisha ukusanyaji wa maoni ya watalii 2,530 yaliyokusanywa kutoka tovuti ya SafariBookings.com.
Maoni 1670 yalitolewa na watalii kutoka nchi 72 duniani kote. Idadi iliyosalia ilichangiwa na wataalamu wa sekta ya utalii.
Image captionSimba ni miongoni mwa wanyama watano wakubwa wapatikanao hifadhi ya Serengeti
Moja ya sababu za hifadhi hiyo kuwa bora zaidi ni uwepo wa wanyama wengi wakiwemo aina tano kubwa (Big Five) ambao ni Tembo, Simba, Faru, Chui na Nyati.
Sababu nyingine ni kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni limetaja eneo hilo kuwa urathi wa dunia.
Mbuga hiyo ni rahisi kutembelewa na watalii kutoka ng'ambo.
Kuhama kwa wanyama zaidi ya milioni moja kila mwaka pia kumefanya mbuga hiyo kuwa kivutio kwa watalii.

No comments :

Post a Comment